Ivory Coast washindi wa kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2015.
Leo hii Februari 12,2015,FIFA imetoa Listi ya Ubora Duniani na zile Nchi 5 Bora, zikiongozwa na Mabingwa wa Dunia Ujerumani ziko Nafasi zao zile zile huku Tanzania ikiporomoka Nafasi 3 na kushika Nafasi ya 107. Ivory Coast imepanda katika orodha ya shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu.
Equitorial Guinea waandalizi wa kombe hilo pia walipanda na kuorodheshwa miongoni mwa mataifa 50 bora duniani.
Kikosi hicho kilipanda nafasi 69 na sasa kiko sawa na Congo DR katika nafasi ya 49 baada ya kufika nusu fainali ya mchuano hiyo japo kwa utata.
Kikosi cha timu ya Algeria bado kinaongoza barani afrika kulingana na orodha mpya ya FIFA.
Kwa Bara la Afrika, Nchi ya juu kabisa bado ni Algeria ambayo iko Nafasi ya 18 wakifuatiwa na Mabingwa Wapya wa Afrika 2015 , Ivory Coast, ambao wako Nafasi ya 20, wakati Ghana, waliofungwa na Ivory Coast kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, wameruka Nafasi 12 na sasa wapo Nafasi ya 25.
Ujerumani yaendelea kuongoza katika orodha mpya ya fifa baada ya kushinda kombe la dunia 2014.
Mataifa yalioshuka vibaya katika orodha hiyo barani Afrika ni Libya ilioshuka nafasi 35 hadi nambari 113 duniani.
Listi ya Ubora Duniani inayofuata itatolewa Machi 12.
10 BORA YA AFRICA.
1. Algeria 2. Ivory Coast 3. Ghana 4. Tunisia 5. Cape Verde 6. Senegal 7. Nigeria 8. Guinea 9. Cameroon 10. Congo DR.
10 BORA DUNIANI.
1. Germany 2. Argentina 3. Colombia 4. Belgium 5. Netherlands 6. Brazil 7. Portugal 8. France 9. Uruguay 10. Spain.