Sherehe za maadhimisho hayo inazoendelea hivi sasa zinafanyika katika uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mgeni rasmi ambaye tayari amewasili viwanjani hapo ni mwenyekiti wa chama hicho Dkt Jakaya Kikwete ambaye tunatarajia atazungumza mengi kuhusu chama na taifa kwa ujumla.
Burudani mbalimbali zimepangwa kutumbuiza zikiongozwa na Kapten John Komba akiwa na bendi zake za TOT pamoja na Diamond Platnums.