Ghana imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2015 baada ya kuwachapa wenyeji Equatorial Guinea mabao 3-0 katika mchezo wa Nusu Fainali uliochezwa jana.Magoli ya Ghana yalifungwa na Jordan Ayew dakika ya 42, Wakaso Mubarak dakika ya 45 na Andrew Ayew dakika ya 75.
Kwa matokeo hayo sasa Ghana itakutana na Ivory Coast katika mchezo wa Fainali utakaopigwa siku ya Jumapili Februari 8, 2014.
Ivory Coast waliwatoa Congo DR kwa mabao 3-1 jana.

Hata hivyo mchezo wa leo kati ya Ghana na Equatorial Guinea ukiwa dakika za mwisho, umeingia dosari baada ya kulazimika kusimama kwa karibu dakika 30 kufuatia vurugu zilizofanywa na mashabiki uwanjani hapo.
Inasadikiwa kwamba baadhi ya mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Ghana walishuka hadi katika eneo la uwanja, na ndipo mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Equatorial Guinea wakaamua kuwafanyia vurugu kwa kuwarushia chupa za maji, hali iliyozua mtafaruku, na ndipo mwamuzi akaamua kusimamisha mchezo.

Baada ya muda,polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya mashabiki waliokuwa wakihusika na vurugu hizo, na baada ya dakika chache hali ilikuwa shwari na mchezo kuendelea kwa kumalizia takribani dakika zisizozidi Tano.
 
Top