Watu wawili wamekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari dogo lenye namba za usajili T 346 DAA leo Januari 31,2015 katika eneo la Lemela ,katika barabara ya Kabanga-Ngara wilayani Ngara mkoani Kagera.



Pichani ni gari hilo dogo aina ya Saloon likiwa limeharibika vibaya baada ya kugonga watu wawili leo Januari 31,2015 na kufa papo hapo eneo la Lemela mjini Ngara.
Askari wa usalama Barabarani akipatia ushahidi wa baskeli iliyoharibika vibaya baada ya kugongwa na gari dogo aina ya Saloon lenye namba za usajili T 346 DAA katika eneo la tukio na kuvipeleka kituo cha Polisi.
Pichani ni miili ya watu wawili waliofariki dunia papo hapo leo Januari 31,2015 baada ya kugongwa na gari dogo aina ya Saloon ,majina ya marehemu hao hayakupatikana mara moja na kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi,chini ni Baiskeli aliyokuwa ikitumiwa na Marehemu hao ikiwa imeharibika vibaya.


 
Top