Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa katika manispaa ya Kigoma-Ujiji mkoani Kigoma baada ya kutokea ajari ya gari aina ya hiace iliyokuwa ikiikwepa gari ndogo aina ya Noah bila mafanikio na kuingia kwenye mtalo huku ikiigonga gari ile ndogo kwa nyuma.
Ajari hiyo ilitokea jana majira ya saa nane mchana maeneo ya Mlole sabasaba baada ya hiace lililokuwa likielekea kijiji cha Msimba Wilaya ya Kigoma vijijini na kabla haijatoka nje ya mji ndipo gari dogo aina ya Noah ilikuwa ikingia barabara kuu hivyo katika jitihada za dereva wa Hiace kutaka kulikwepa akajikuta akiingia kwenye mtalo hata hivyo aliigonga noah kwa nyuma.

Baada ya ajari hiyo Dereva wa Noah iliyogongwa alifariki dunia huku abiria 19 waliokuwa kwenye Hiace walijeruhiwa na kufikishwa katika hospitali ya mkoa Maweni kwaajiri ya matibabu.
 
Kigoma24hours ilifika katika hospitali hiyo ili kuongea na majeruhi kwa lengo la kujua hari zao na nini chanzo cha ajari hiyo ambapo, Jamali Adamu ambaye ni konda wa Hiace lile, alisema kuwa awali aliona gari dogo likiingia barabarani ndipo dereva wa hiace alipojaribu kulikwepa wakajikuta wakiangukia kwenye mtalo.


Adamu aliiambia Kigoma24hours kuwa baada ya kuanguka alikuwa hajiwezi ila aliona watu wakimbeba kwenye mabega na kumweka kwenye gari ambapo alipelekwa moja kwa moja Hospilalini kwaajiri ya matibabu kwani aliumia sehemu ya chini ya mdomo huku akijisikia maumivu kichwani.

Aidha Asha Deo alisema kuwa wakati wakiwa kwenye safari dereva alikuwa akiendesha gari kwa kasi japo abiria walimwambia apunguze mwendo ila hakupunguza ndipo ilipotokea gari nyingine na kutaka kuigonga akapeleka gari kwenye mtalo.

“Ajari hii ni sababu ya mwendo kasi kwani kama dereva angesikia alivyokuwa akiambiwa na abiria tusingepata ajari, lakini alipoambiwa yeye alituuliza kuwa hamtaki kuwahi kufika, huku akiendelea kuongeza mwendo” alisema Deo.

Pia Ahmad Samweli ambaye ni mkazi wa Msimba alisema kuwa walipoanza safari gari lilikuwa katika mwendo huku Hiace walilopanda lilikuwa likifukuzana na gari lingine ila hawakujua kinachoendelea nje kwani walikua viti vya nyuma ndipo wakasikia mshindo mkubwa na kushitukia wako mtaloni.

Nae Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Maweni, Fadhiri Kibaya alisema kuwa baada ya ajari hiyo walipokea majeruhi 19 na mtu mmoja aliyekuwa ameshafariki alifikishwa moja kwa moja mochwari.

“Katika idadi hiyo ya majeruhi wanaume wako 9 na wanawake 9 huku akiwemo mtoto mdogo aliyekuwa amebebwa na mama yake kabla ya ajari na wote hao wako wodini kwaajiri ya matibabu ila mwili wa marehemu unasubilia ndugu zake kwaajiri ya taratibu za mazishi” alisema Kibaya.

Hata hivyo Kibaya alisema kuwa yupo mgonjwa mmoja ambaye ni mahututi ambaye alichomwa na chuma kwenye paji la uso na kikabaki palepele usoni hivyo yuko chumba cha upasuaji kwaajiri ili kuondolewaa chuma hicho.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Hapa, Kamishina Msaidizi ACP, Japhar Muhamed alithibitisha kutokea kwa ajari hiyo na taratibu za uchunguzi zinafanyika ili kupata taarifa kamili.

Chanzo:Emmanuel Senny Kigoma via Kigoma 24hours 
 
 
Top