Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Salmin Awadh enzi za uhai wake.
Taarifa toka visiwani humo zinasema kuwa, Mheshimiwa Salmin Awadh ambaye pia alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, amefariki dunia wakati akishiriki kikao cha CCM kilichokuwa kinafanyika katika ofisi kuu ya chama hicho Kisiwandui.
Alithibitishwa na daktari kuwa amefariki dunia mara baada ya kufikishwa hospitali.
Mwili wa marehemu, Salmin Awadh ukiwekwa kwenye gari ukitolewa kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja kwenda nyumbani kwake kwa matayarisho ya mazishi.
Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Salmin Awadh amefariki dunia ghafla leo akiwa katika Kikao cha Kamati Kuu Zanzibar, katika ofisi kuu ya chama, Kisiwandui.
Mheshimiwa Awadh alizaliwa Juni 26 mwaka 1958 na alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Makunduchi na Kiongoni kati ya mwaka 1963-1970.
Marehemu aliwahi kufanya kazi katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwa na cheo cha Sajenti kati ya mwaka 1976 hadi 1986.
Hadi wakati mauti yanamkuta alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Gazeti la Zanzibar Leo, nafasi aliyokuwa nayo tokea mwaka 2009.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndg Vuai Ali amesema marehemu alifika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kwa kazi zake na kuhidhuria Kikao cha Sekreteli kilichofanyika asibuhi hofisini hapo , na kusema marehemu ametoka chumba cha mkutano na kwenda Afisi kwake ya Mnadhimu wa CCM Baraza la Wawakilishi, ndipo matatizo yalipojitokeza na kusema anajikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa matibabu , kufika huko hali ilibandilika na kufariki dunia.
Marehemu ameacha pigo kwa Chama na wananchi wa jimbo lake.