|
Timu nzima ya redio free afrika na star Tv ikiiongozwa na Mtani Wambura ikiingia uwanjani |
Jana tarehe 14/02/2014 maarufu kama siku ya valentine day au siku ya wapendanao kwa lugha ya kiswahili ilikuwa poa kwa wakazi wa mji wa Kahama ambapo walipata burudani kupitia tamasha la miaka 20 ya kuanzishwa kwa redio free afrika (RFA) ambapo timu ya wafanyakazi wa redio free afrika, na kituo cha Tv cha Star Tv walijumuika pamoja na wafanyakazi wa kituo cha redio cha Kahama Fm katika uwanja wa halmashauri ya mji wa Kahama maarufu kama uwanja wa taifa .
|
Futuhi wakifanya yao uwanjani |
Katika uwanja huo burudani mbalimbali zilitawala ambapo
kwanza kabisa watoto walianza kwa kushindana kucheza mziki, hata hivyo
wacheza karatee hawakuwa mbali walionesha mambo yao. Baraka za mvua
hazikuwa mbali na mji huo ilinyesha mvua kubwa iliyosababisha michezo
kusitishwa kwa muda lakini baaada ya mvua kutulia, futuhi waliingia
uwanjani na kutoa burudani ya vichekesho kwa wakazi wa mji wa Kahama na
baada ya futuhi ulifatia mtanange wa mpira wa miguu kati ya timu ya
Redio free afrika na timu ya Kahama Fm ambapo katika mchezo huo ulokuwa
wa kuvutia kwa watazamaji hakuna timu iliyoibuka mbabe japo timu ya
Kahama Fm ilitumbukiza mipira miwili gorini lakini yote mshika kibendera
alikataa kuwa sio gori, hadi dakika ya mwisho wa mchezo timu zote
zilitoka uwanjani kwa suluhu ya bila kufungana na hivyo kupelekea
nahodha wa timu zote mbili kukubaliana kurudia tena mchezo huo siku
nyingine.
|
Futuhi wakifanya yao |