Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (kushoto) akiwa katika kutazama mashine zinazozalisha Umeme zilizopo eneo la Nakatunga ,wilayani Ngara mkoani Kagera hivi karibuni alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo.
Juu na chini ni Naibu Waziri Mwijage aliyevaa vizuia sauti kali masikioni,akikagua Mtambo wa kufua Umeme namba mbili wa shirika la umeme TANESCO wilayani Ngara mkoani Kagera ambao umekua uko katika matengenezo yasiyoisha sasa na hivyo kusababisha kuwepo kwa mgao wa umeme wa mara kwa mara kwa wateja kwani Mashine namba moja imekua ikizidiwa Matumizi.



Baadhi ya wakazi wa Mji mdogo wa Ngara Mkoani Kagera wakiwemo wafanyabiashara, wamelilalamikia shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO wilayani Ngara kwa kuwa na upendeleo katika utoaji wa huduma ya nishati ya umeme.

Wakiongea na Redio Kwizera, wakazi hao wamedai kuwa wanashindwa kutambua mgawanyo wa umeme unavyofanyika katika kipindi cha mgao, kwani baadhi ya watumiaji wanapata umeme kwa zaidi ya siku tatu mfululizo wakati wengine wakikosa huduma hiyo kwa siku kadhaa

Bi Jacquiline Ntamalengelo mmliki wa saluni ya kike mjini Ngara, amesema mkatiko wa umeme wa mara kwa mara umeathiri biashara yake kwa kiasi kikubwa kutokana na kutokuwa na umeme wa kuaminika

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANESCO wilayani Ngara Bw Mshumbusi Fransisi alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia madai hayo, amedai kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yuko nje ya Ofisi kikazi.

Aidha March 10,2015,Shirika hilo la Umeme TANESCO wilayani Ngara kupitia Uongozi wake walitoa TANGAZO kwa wateja wao kuhusu matengenezo ya Mtambo wake wa kufua Umeme namba mbili kufikia hatua nzuri ya matengenezo,hivyo kutarajia kuwa makali ya umeme kupungua kuanzia March 12,2015 lakini hali ya mgao wa mara kwa mara wa muda mrefu katika baadhi ya maeneo wilayani humo umeripotiwa kuendelea hadi sasa.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ngara ,mkoani Kagera mara baada ya kuwasiri kwa ziara ya siku moja hivi karibuni.

 
Top