Kwa mujibu wa Katiba ya ACT ZZK atakuwa na madaraka yafuatato
"Kazi za Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania
i) Atakuwa kiongozi mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa, mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.

ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na
mwelekezaji kwa viongozi wote na
maafisa wa ACT-Tanzania

iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii
iv) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama

v) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.

vi) Atasimamia, kufunza na kutoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-Tanzania

vii) Iwapo kiongozi wa ACT-Tanzania hayupo kwa sababu yoyote ile basi
Mwenyekiti wa chama Taifa atakuwa Kaimu kiongozi mkuu wa Chama.

viii) Iwapo kiti cha kiongozi mkuu wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya
kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama,
maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, utaratibu
ulioelezwa katika

(vi) ya ibara ndogo hii utatumika kwa sharti kwamba Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi sita tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi Mkuu wa Chama mwingine.

ix) Ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya
Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la

Mkutano Mkuu wa Taifa litakaloungwa mkono na theluthi mbili ya kura za wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura.
x) Atakuwa ni nuru na taswira ya ACT-
Tanzania"

 
Top