Matumla akiendelea kuwafurahisha mashabiki wake Watanzania waliofurika ukumbini wakati alifanya kazi kubwa na ya ziada kumshinda Mchina Xin Huaambaye alionyesha kiwango kizuri.
Ushindi wake wa pointi kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, hakuwa na ubishi.
Bondia Mohamed Matumla, akiwa amebebwa juu na mashabiki wake baada ya kutangazwa mshindi katika pambano lake la kimataifa la raundi 10 na Bondia Xin Hua kutoka nchini China lililomalizika usiku wa March 27,2015, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Katika pambano hilo Matumla Jr, alionekana kumzidia Mchina huyo aliyekuwa akilalama muda wote kuwa anachezewa rafu na mpinzania wake.
Na katika mapambano mengine ya utangulizi, Thomas Mashali kwa mara nyingine tena ameingia mitini kumkacha mpinzani wake Karama Nyilawila, ambaye ilibidi abadilishiwe bondia na kupigana na Ibrahim Tamba, ambaye pia alimshinda kwa KO katika raundi ya mwisho ya nane.
Pambano jingine lilikuwa ni kati ya Japhet Kaseba, aliyepigwa kwa KO na Mada Maugo katika raundi ya saba kati ya nane zilizokuwa zimepangwa kuchezwa, huku pia Ashraf Suleiman, naye akimchapa mpinzani wake Bernard Adie, kutoka nchini Kenya kwa KO katika raundi ya tatu, ambapo Bondia kutoka Mrekani aliyekuwa acheze na Ashraf, imeelezwa kuwa hakuweza kufika kutokana na sababu kadha wa kadha zilizomkwamisha.
Na katika pambano la raundi nane lililokuwa la kuwania ubingwa kwa mabondia wanawake kati ya Bena Kaloki kutoka Kenya na Asha Ngedele, lilimalizika kwa Mkenya kutwaa ubingwa huo kwa kumchapa Mtanzania kwa KO katika raundi ya nne.