Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Arsenal jana April 18, 2015 wakicheza Uwanja wa Wembley Jijini London, waliichapa Timu ya Daraja la chini la Championship, Reading Bao 2 - 1 katika Nusu Fainali ya kombe hilo.
Pasi safi ya Mesut Ozil ndiyo iliyompa nafasi Alexis Sanchez kuipa Bao la kwanza Arsenal Dakika ya 30 Bao ambalo lilidumu hadi Mapumziko.
Reading walisawazisha katika Dakika ya 54 kwa Bao la McCleary alieunganisha krosi ya Pogrebnyak kutoka kushoto kwa goli.
Hadi Dakika 90 kumalizika Gemu ilikuwa 1-1 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.
Alexis Sanchez aliipa Arsenal Bao la Pili na la ushindi katika Dakika ya 106 baada ya Shuti lake kumpenya Kipa Federici.
Nusu Fainali nyingine itachezwa leo Jumapili April 19, 2015, pia Uwanjani Wembley, kati ya Aston Villa na Liverpool.KUCHEKI PICHA ZAIDI ZA MCHEZO HUU..BOFYA HAPA