Viongo walivyokamatwa navyo watuhumiwa hao.
Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuwakamata watu 6 na tuhuma za kukutwa na viungo vya Albino wakiwa katika harakati za kuviuza viungo hivyo.
Akizungumza na Dunia Kiganjani Blog ofisini kwake mkuu wa kituo cha Polisi wilayani Kahama Leonard Nyandahu, amesema watu hao wamekamatwa jana majira ya saa 7 mchana katika nyumba ya kulala wageni ya MAJI HOTEL, iliyopo Phantom kata ya Nyasubi wilayani Kahama.
Nyandahu amewataja watu hao kuwa ni Bahati Kirungu(56) mwalimu wa shule ya msingi Katungulu kata ya Wendele,Mhoja John(24) mkulima mkazi wa Isagehe Nzega,Bilia Busanda(39) mkulima mkazi wa Mogwa Nzega.
Wengine ni Shija Makandi(60) mkulima mkazi wa Isagehe Nzega,Regina Kashinje(40) mkulima mkazi wa Isagehe Nzega,na Aboubakary Ally(25) ambaye ndiye aliyewahifadhi watu hao mkazi wa Isagehe Nzega.
Nyandahu amesema mnamo tarehe 19.5.2015 asubuhi mkuu wa upelelezi kituo cha Polisi Nzega alipata taarifa za mtu kuwa anauza viungo vya Albino na mtego wa kumkamata ulifanyika bila mafanikio badala yake akahamishia biashara hiyo wilayani Kahama.
Aidha Nyandahu amesema maafisa upelezi mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Afsa upelelezi kituo cha polisi Kahama walifuatilia nyendo za watu hao na ndipo mtego wa kuwakamata watu hao ulipowekwa na kuwanasa.
Hata hivyo Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linaendelea kuwashikilia watu hao kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kuubaini mtandao wao pamoja na hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Chanzo: Kiganjani Blog