Kikao hicho kilifanyika siku ya Jumapili ya tarehe 24/05/2015 maeneo ya Ilala Boma katika ukumbi wa Ramada Hotel. Kikao kilianza na ajenda ya ufunguzi kwa kusoma musitsari wa kikao kilichopita ambapo bwana Aberi Ngwebe aliteuliwa na mwenyekiti wa umoja huo kusoma muhitsari huo kwa niaba ya katibu bwana Asheri Majanja ambaye hakuhudhuria kwa dharura ya kuwa safarini kikazi.
Kikao hicho kilikuwa na ajenda kuu mbili yaani kusoma na kupitisha katiba ya umoja huo na kuchagua uongozi, hata hivyo zoezi la kuchambua katiba lilichukua muda hivyo zoezi la kuchagua uongozi halikufanyika kabisaa kwa siku hiyo, kutokana na wajumbe wengi kulidhishwa na vipengere vya katiba hiyo na huku mapungufu yakiwa machache waliazimia kuirekebisha ili kuondoa mapungufu hayo na hivyo kufikia tarehe 07/06/2015 wanaumoja wote watakutana ili kuipitisha katiba hiyo.
Aidha wajumbe wengi walifurahia zaidi sura ya kwanza ya katiba hiyo ibara ya pili ambayo inasema kwa ufupi kuwa ina malengo ya kuchochea maendeleo ya wilaya ya Ngara, kufahamiana, kusaididana kutatua matatizo mbalimbali, kubuni na kuboresha miradi mbalimbali kwa manufaa ya umoja na jamii nzima ya wanangara,kuboresha sekta mbalimbali wilayani Ngara kama vile elimu, afya , usafiri, kilimo, ufugaji na utamaduni bila kusahau masuala ya nidhamu ambapo kikatiba sura ya sita ya katiba ya umoja huo inawapa mamlaka wazee wa umoja huo kuwaadhibu vijana watakaoenda kinyume na maadili ya wananagara.
Mwisho mwenyekiti wa kikao aliwasihi wanangara kudumisha umoja na ushirikiano huku akiwaomba hata wale ambao ni wanangara waliopo Dar es salaam wajitokeze na kujiunga na umoja huo ili malengo ya umoja yafanikiwe.

 
Top