Taarifa za mwanzo kutoka mkoani Dodoma zilisema kuwa Basi la SIMIYU EXPRESS lilipata ajali eneo la Chalinze - Mbande mkoani Dodoma Jioni ya jana July 22, 2015 na Abiria takribani 8 walifariki dunia, huku zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa baada ya basi hilo walilokua wakisafiria kutoka Jijini Mwanza kwenda Dar es Salaam kupasuka tairi la mbele kushoto na kupoteza uelekeo na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.
Pichani ni muonekano wa basi hilo la SIMIYU EXPRESS likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali .
Baadhi ya majeruhi ambao walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma.