Wafuasi wa Mgombea Udiwani kata ya Rusumo ,wilayani Ngara mkoani Kagera anayetetea kiti hicho kwa mara nyingine kwenye Uchaguzi Mkuu 2015,Bw.Wilbard Mbambara wakiwa na shamrashamra baada ya kumsindikiza kuchukua na kurudisha fomu ya kuwania Kiti hicho hapo Jana Julai 19,2015 kwenye ofisi za CCM kata ya Rusumo-Picha kwa hisani ya Seif Omary Upupu-Ngara.
Bw.Wilbard Mbambara akiwa na fomu za kuomba kuwania Udiwani mara baada ya kuchukua ,kulia kwake ni Bw.Thomson Seyongweambaye amestaafu Udiwani ,Kata ya Kirusha.

Bw.Wilbard Mbambara akizisoma kwa umakini fomu pamoja na kuzijaza ili kuomba ridhaa ya CCM kumchagua kusimama kukitetea kiti cha Udiwani wa Kata ya Rusumo kwa mara nyingine tena.

Baada ya mchakato wa kuwania Urais, sasa vita ya Uchaguzi Mkuu 2015 imehamia kwenye Ubunge na Udiwani hasa kutoka katika vyama vikubwa vya CCM kinachotawala na CHADEMA kinachoongoza Upinzani.

Hadi jana Julai 19,2015, ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho kwa Chama cha Mapinduzi CCM kuchukua na kurejesha fomu.

JIMBO LA NGARA,MKOANI KAGERA .
Walioomba ridhaa ya CCM ni Wagombea 9 ambao ni:-

Dr.Philmoni Sengati.

Cyprian Muheranyi.

Bi.Hellena Adrian Ghozi.

Wilbard Eden Ntamahungiro.

Alex Rafael Gashaza.

Jerad Muhile.

Joachim Nchunda.

Issa Samma.

Na – Ladislaus Bambanza.
Kwa upande wa Madiwani waliochukua fomu na kurudisha ndani ya CCM, Jumla yao ni 62,waliopita bila kupingwa ndani ya kata zao kupitia CCM ni:-

Kata ya Kasulo – Philbert Kiiza.

Kata ya Murusagamba - Soud Mkubila.

Kata ya Bugarama – Adronizi Bulindoli.

Kata ya Murukulazo – Mukiza Byamungu.
Mara baada ya zoezi hilo kukamilika,kwa upande wa nafasi za Ubunge na Udiwani ,Kampeni za ushawishi kwa wanachama wa CCM kwenye matawi zitafanyika kuanzia tarehe 20 mpaka 31 Julai 2015 ambapo kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea katika ngazi hizo zitapigwa sambamamba tarehe 1/08/2015.
 
Top