Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Januari Makamba amesema Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imefanya maamuzi sahihi ya kutangaza tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi na hakuna mwenye uwezo wa kuhoji hatua hiyo.
Waziri Makamba ameyasema hayo alipokuwa akihitimisha hotuba ya waziri Mkuu kwa upande wa wizara yake ya Muungano na mazingira baada ya kujadiliwa na Wabunge.

Kwa mujibu wa Katiba ibara ya 119 (10) Tume ya Uchaguzi imepewa uhalali wa kufanya maamuzi kwa mustakabali wa taifa letu, pia kikao kilichokaa na kuamua tarehe ya kurudia uchaguzi wa Zanzibar akidi ilikidhi vigezo hivyo uchaguzi huu upo kisheria na utafanyika kama ulivyopangwa.

Aidha waziri ametoa wito kwa upande wa upinzani kwamba wakubali kuheshimu sheria na taratibu za nchi na huko wanakokwenda kulalamika hawatapata faida yoyote na wenye uwezo wa kuleta amani ndani ya nchi hii ni sisi wanasiasa wa hapa hapa nchini.
 
Top