Mabingwa wa Ligi Daraja la 3 Mkoani Kagera –Timu ya Murusagamba FCPichani na wenzao Washindi wa Pili Nzaza Stars hii leo,March 25,2016 wamewasili salama hapa wilayani Ngara wakitokea huko wilayani Misenyi mkoani Kagera ambako hapo Jana walicheza Mchezo wa fainali wa mashindano hayo na Murusagamba FC kuibuka na zawadi hiyo ambayo waliitafuta kwa kipindi sasa toka mwaka 2013 walipoibuka kuwa Mabingwa wa wilaya ya Ngara na kuwafunga ndugu zao Nzaza Stars bao 1 – 0 katika mchezo uliochezwa jioni ya jana katika uwanja wa mashujaa Bunazi wilayani Misenyi.

Pichani katikati ni Mbunge wa jimbo la Ngara ALEX GASHAZA ( CCM ), Mkuu wa wilaya ya Ngara ,mkoani Kagera-HONORATHA CHITANDA kulia na kushoto kwao Mwenyekiti wa chama cha Soka wilaya ya Ngara NDFA –Godfrey Brayan katika Hafla fupi ya kuwapongeza Mabingwa wa Mkoa wa Kagera 2016/2017 Murusagamba FC Baada ya kuwasili hapa mjini Ngara majira ya saa 5 asubuhi leo March 25,2016, Timu hizo zote ziliandaliwa Mapokezi hayo yakiongozwa na Mkuu wa wilaya,Mbunge, Mwenyekiti wa Halmashauri ERICK NKILAMACHUMU sambamba na wadau mbalimbali wa michezo.

Pamoja na mambo mengine, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara,ERICK NKILAMACHUMU , Mbunge ALEX GASHAZA,Chama cha soka –NDFA na Wadau mbalimbali wa michezo katika salamu zao za Pongeziwamekubaliana kuandaa/kuboresha uwanja wenye kukidhi viwango utakaohimili mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa baada ya kutoa Bingwa wa Mkoa wa Kagera ili kituo cha Mashindano hayo kiwepo Wilayani Ngara badala ya Mjini Bukoba katika uwanja wa Kaitaba.
 
Top