Timu ya mpira wa miguu ya Nzaza Fc kutoka wilayani Ngara inayoshiriki ligi ya Mkoa wa Kagera ilianza vema mchezo wake wa kwanza kwa kuwafunga wenyeji timu ya Muleba fc jumla ya goli tatu (3) kwa moja (1) katika uwanja wa vijana wa halmashauri ya mji mdogo wa Muleba.
Mchezo huo wa uzinduzi wa ligi ya mkoa wa kusaka bingwa wa mkoa ulichezwa jana jumamosi ya tarehe 05/03/2016 ambapo timu ya Nzaza fc ilifungua dimba na timu ya wenyeji wa mashindano hayo Muleba fc, katika mchezo huo timu ya Nzaza fc ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao Salumu Mkamate(Rasta) na baadae wenyeji muleba fc walisawazisha goli hilo kupitia mkwaju wa penati baada ya beki wa Nzaza kumfanyia madhabi ndani ya kumi na nane mchezaji wa Muleba fc. Baadae kidogo kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Nzaza fc walipata goli la pili kupitia kwa mshambuliaji wao huyo huyo Salumu Mkamate hivyo na kufanya timu zote kwenda mapumziko matokeo yakisomeka Nzaza goli mbili na Muleba fc goli moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu ila bahati haikuwa kwa wenyeji ambapo timu ya Nzaza fc ilifunga goli ya tatu kupitia kwa mshambuliaji wao John Buguba hivyo na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa jumla ya ushindi wa Nzaza fc wa goli tatu kwa moja.
 
Top