Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo tarehe 29/04/2016 katika kijiji cha Ibuga ambapo inasemekana kijana aliyefahamika kwa jina la Balenga Josias Joakim alivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha (bunduki) muda wa usiku akielekea kwake ambapo alikimbia na kupigwa risasi kadhaa zilizopelekea kupoteza maisha, lakini pia katika sakata hilo majambazi hao wamejikuta wakimpiga risasi jambazi mwenzao aliyekuwa akimkimbiza Balenga kipindi akijaribu kujinasua mikononi mwa majambazi hao.
Jeshi la polisi la kituo cha Kabanga limethibithisha tukio hilo na mtu mmoja ameshikiliwa kwa upelelezi zaidi baada ya wananchi kumshtukia akionekana maeneo ya tukio asubuhi sana huku akiwa si mwenyeji wa eneo hilo na maelezo yake yakiwa hayaeleweki vizuri haijajulikana kama ni mhusika wa tukio hilo au laa.
 
Top