Muonekano wa barabara ya Rusumo - Nyakahura-Lusahunga inayounganisha Nchi ya Tanzania na Rwanda kupitia Daraja la Kimataifa la Rusumo lililopo wilayani Ngara mkoani Kagera. 
Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB imetoa Msaada wa Dola Milioni 156 za Marekani kwa Tanzania na Rwanda kwa ajili ya matengenezo ya Barabara ya Lami yenye urefu wa Kilomita 402 ili kuharakisha maendeleo ya Kibiashara kwa nchi hizo
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha Kutoa Huduma za Pamoja cha Forodha kwenye Mpaka wa Rusumo,wilayani Ngara mkoani Kagera Jana ,April 06,2016,baina ya nchi hizo Mbili za Tanzania na Rwanda, Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Bi Tunia Kadiero amesema kwa upande wa Rwanda hiyo ni kutoka Kibuye – Busega – Mpigi hadi Kitumbayenye urefu wa Kilomita 241 .

Muonekano wa Daraja la Kimataifa la Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda, kushoto ni daraja la zamani lenye rangi ya njano na kulia ni Daraja jipya.

Amesema kwa Nchi ya Tanzania, Barabara hiyo ni kutoka Lusahunga hadi Rusumokuelekea barabara ya Kayonza nchini Rwanda yenye urefu wa Kilomita 161na kwamba matengenezo hayo yatakamilika ndani ya Miezi 8.

Rais wa Tanzania,Dr John Pombe Magufuli amesema pamoja na ujenzi wa barabara katika Nchi za Afrika ya Mashariki, Serikali ya Tanzania itaendelea na mpango wake wa kujenga Reli inayounganisha nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi katika kusafirisha mizigo na kuwataka raia wa nchi zote kuitunza miundombinu hiyo.
 
Top