JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
Anwani ya Simu: “REGCOM”
Simu ya mdomo: (028) 2220215-18
E-mail:ras.kagera@pmoralg.go.tz
Fax: (028) 2222341 / 2221356
OFISI YA MKUU WA MKOA,
S. L. P. 299,
BUKOBA - KAGERA.
TANZANIA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 11 JULAI, 2O16
Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Harrison Mwakyembe anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kagera kuanzia tarehe 14-16 Julai, 2016.
Siku ya kwanza ya tarehe 14 Julai, 2016 Mhe. Mwakyembe anatarajia kukutana na kuongea na wadau waliopo chini ya Wizara yake ya Sheria na Katiba pamoja na Vyombo vya Habari katika Ukumbimbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuanzia saa 6:00 hadi saa 7:00 Mchana. Aidha kuanzia saa 7:30 hadi 8:30 mchana atatembelea ofisi za RITA kujionea uandikishaji wa watoto waliochini ya miaka mitano.
Katika siku ya pili ya tarehe 15 Julai, 2016 Mhe. Mwakyembe atatembelea Gereza la Wafungwa la Mkoa wa Kagera, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Manispaa ya Bukoba ili kuongea na uongozi wa ofisi hizo ambazo zipo chini ya Wizara yake.
Siku ya tatu ya tarehe 16 Julai, 2016 Mhe. Mwakyembe akiwa mkoani Kagera ataelekea Wilayani Biharamulo ambapo atatembelea Gereza la Wafungwa Biharamulo na kuhitimisha ziara yake katika Mkoa wa Kagera na kuondoka kuelekea Mkoani Mwanza.
Sylvester Raphael
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
11 Julai, 2016
