Ajari hiyo imetokea eneo la shule ya Msingi Kanazi ambapo mwendesha baiskeli huyo alikuwa barabarani akitokea mashineni na lori hilo lilikuwa likitokea Kabanga Ngara, dereva wa lori hilo amejaribu kumkwepa mtu huyo lakini jitihadi zake hazikufanikiwa maana mwendesha baiskeli amejigonga kwenye gari hilo na kufariki hapo hapo naye amejikuta anatumbukiza lori hilo kwenye Korongo.
Akieleza dada mmoja (jina lake halikufahamika hapo hapo) aliyekuwa kwenye lori hilo amesema mwendesha baiskeli amenyumbayumba sana mbele yao hali iliyopelekea dereva huyo kumkwepa mara mbili bila mafanikio na kujikuta wakihama barabara na kutumbukia kwenye korongo pembeni mwa barabara, dereva amekimbia kuepuka hasira za wanachi.