Mwanariadha kutokea nchini Jamaica, Usain Bolt, amedhihirisha kwamba yeye ni mwamba wa mbio za Mita fupi mara baada ya kushinda Mita 200 katika michuano ya Olimpic inayofanyika huko Rio nchini Brazil na kujinyakulia medali ya Dhahabu ikiwa ni mara ya pili baada ya kunyakua ya michuano yam bio za Mita 100.
Bolt aliweza kushinda mbio hizo kwa urahisi kwa kutumika Sekunde 19.79 na kwa sasa anahitaji kushinda mbio za mita 400 za kupokezana vijiti ili kukamilisha medali ya tatu ya dhahabu kama alivyofanya katika michuano iliyopita.
Mapema wiki hii alidhihirisha kuwa ni mwamba wa mbio fupi pale aliposhinda mbio za mita 100 na kunyakuwa medali ya dhahabu.
Kwa upande wa Marekani imeweza kujinyakulia medali nyingine nne za Dhahabu ikiwemo ya mwanariadha wake Ashton Eaton.
Huku mkimbiaji kutokea nchini Kenya aliyekuwa ametangaza kustaafu, Ezekiel Kemboi, ameeleza kwamba ameahirisha kustaafu mara baada ya kunyang`anyway medali aliyokuwa ameshinda katika mbio za kuruka viunzi na maji.
Medali hiyo iliyochukuliwa na Mfaransa mara baada ya kukata Rufaa kwenye Mita 3000 imemfanya Kemboi kusema kuwa watakutana tena London 2017 kwenye michezo ya Olimpiki ili kuweza kudhihirisha kwamba alikuwa akistahili medali hiyo.