Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania, Mhe.Mwigulu Nchemba akiongea LIVE katika studio za RADIO KWIZERA FM-NGARA alipofanya ziara wilayani Ngara mkoani Kagera leo Agosti 11,2016.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bw Mwigulu Nchemba katika Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa radio Kwizera FM-Ngara/Kagera.
Waziri Nchemba amesema Serikali itatoa Kipaumbele kwa Watanzania wanaoishi maeneo ya Mipakani katika kuwapatia Vitambulisho vya Uraia ili kuwaondolea usumbufu baina yao na Maafisa uhamiaji.
Bw Nchemba ametoa kauli hiyo leo, Agosti 11,2016, Asubuhi wakati akijibu swali katika Mahojiano Maalum na Radio Kwizera kuhusu adha wanayoipata Watanzania wanaoishi mipakani kutoka kwa Askari wa Uhamiaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba katika Picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa Radio Kwizera FM-Ngara/Kagera Padre.Damas Missanga -JRS.
Waziri amesema amewaelekeza Wataalam kupitia Wizara yake kuweka Kipaumbele kwa kuwapa Vitambulisho Watanzania wa Mipakani na kwamba licha ya kuondoa usumbufu huo vitambulisho hivyo pia vitatumika kuimarisha usalama wa taifa.
Katika hatua nyingine , Waziri Nchemba amewataka watumishi wa Serikali walio chini ya wizara yake kuwa waadilifu na kuweka mbele uzalendo hasa kwa Jeshi la Polisi kufanya kazi zao kwa misingi ya kisheria ili kuepuka kuchukiwa na Jamii badala yake Jamii ifurahie uwepo wa Jeshi hilo.
CREDIT: REDIO KWIZERA-NGARA