Kuelekea mchezo wa marudia leo ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali kati ya wenyeji Manchester City dhidi ya Liverpool, hizi ni rekodi ambazo zinaweza kuvunjwa au kuwekwa na timu zote mbili endapo zitapata matokeo chanya.

Katika Historia ya ligi ya Mabingwa ni timu mbili tu ambazo zimewahi kubadili matokeo kutoka kufungwa mabao matatu au zaidi kwenye mchezo wa raundi ya kwanza. Deportivo La Coruna dhidi ya AC Milan mwaka 2003-04 na Barcelona dhidi ya Paris Saint-Germain msimu uliopita.

Hata hivyo Manchester City wanajivunia ushindi wao mnono dhidi ya Liverpool ambapo waliifunga mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza wa ligi uliopigwa kwenye dimba la Etihad. Katika mechi 9 walizokutana hivi karibuni Man City ameshinda mechi hiyo pekee huku wakitoa sare mara mbili na Liverpool kushinda mechi 6.
Liverpool wanaiwinda rekodi yao ya mwaka 2005 ambapo walicheza mechi 6 mfululizo za UEFA bila kupoteza na msimu huo waliibuka mabingwa. Hadi sasa timu hiyo imecheza mechi 5 mfululizo bila kufungwa ikitoa sare 2 na kushinda 3.

Rekodi nyingine kali ambayo Liverpool inaweza kuipata leo ni kuwa timu ya kwanza kuifunga Man City mara tatu mfululizo ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2009 ilipofungwa mara tatu mfululizo na Manchester United.
 
Top