Msichana huyo Rosemary Marwa mkazi wa Musoma ambaye awali alijitambulisha kuwa ni mkazi wa Dar es salaam, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Murgwanza tangu May 28 mwaka huu ,akipatiwa matibabu na ameruhusiwa May 31,mwaka huu baada ya kupon.
Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara ,Bw Abeli Mtagwa amesema kwa sasa msichana huyo bado anahojiwa na polisi na kwamba anatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho (June 03,2014) baada ya upelelezi kukamilika ili ajibu tuhuma zinazomkabili.
Hata hivyo Bw Mtagwa amekemea tabia ya watu kutaka kujiua kwa kisingio cha wivu wa Kimapenzi na Ugumu wa Maisha na kwamba serikali itaendelea kuwachukulia hatua wote watakaobainika kufanya hivyo.
Habari Na:-Radio Kwizera FM.
Habari Na:-Radio Kwizera FM.