Waliofika eneo la tukio
Mawe hayo ya mvua yanadaiwa kuwa na ukubwa wa ndoo ya lita 10,na yalikuwa yamezagaa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika.Pichani ni barafu ikiwa imeanza kuyeyuka


Watu 38 wamefariki dunia na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mwakata Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 
Mbuzi wakiwa wamekufa

 
Mbuzi awakiwa wamekufa

 
Vyakula vikiwa kwenye nyumba iliyoharibika

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya(mwenye suti) amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada. 
eneo la tukio
Viongozi wakiwa eneo la tukio
makazi hakuna Barafu maarufu MAWE ikiwa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika
Hali halisi katika eneo la tukio 

Blog hii imefika katika eneo la tukio na kushuhudia nyumba za kaya mbalimbali katika kijiji hicho zikiwa zimebomoka na nyingine kuezuliwa mapaa huku hali ya mazao na miti ikiharibiwa vibaya na mvua hiyo ambayo pia imeuwa mifugo. 

Moja ya nyumba zilizoharibika
Kijijini Mwakata

majaruba yakiwa yamefurika maji 
madhara ya mvua hiyo
Madhara ya mvua

Mazao shambani 

Miti imevunjika
Eneo la Mwakata

Jinsi Mimea ilivyoharibika

Hali halisi eneo la tukio 
Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha(pichani) amesema waliokufa wengi ni watoto ambao walisombwa na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao na kwamba majeruhi wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Wananchi wakihangaika
Kamanda Kamugisha amesema watu 35 wamekufa eneo la tukio na wengine wamekufa walipofikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wengine kuwa na hali mbaya.





Mpesya amesema majina ya waliokufa kwa sasa bado hayajatambulika na kwamba kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga inakaa jioni hii ili kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa wahanga hao.


Akiwa eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa hayo wakati serikali ikisubiri kukamilika kwa zoezi la sense ya wahanga hao aliloagiza kufanywa na viongozi wa eneo hilo. 
Mwananchi akiwa haamini kilichotokea


 
Top