Kasisi Don

Kasisi mmoja nchini Italia, ameweka kifaa kanisani mwake kinachoweza kubana mawasiliano ya simu baada ya kuchoka kuwaomba waumini kuzima simu zao kila wakati alipokuwa anahubiri.
Alilazimika kuomba idhini ya polisi kuweka kifaa hicho baada ya kuchoka kusikia milio ya simu zikipokea ujumbe.

Mpango huo umesifiwa sana na waumini ingawa imewaudhi wenye maduka katika mji wa Naples wanaosema kifaa hicho kinatatiza masafa na mawasiliano yao na pia kifaa hicho kimeathiri mashine za kutoa pesa.

Wanasema kifaa hicho pia kinatatiza shughuli zao ambapo wateja huagiza bidhaa kupitia simu zao za mkononi.Kasisi Don alikasirishwa sana na waumini wake kujibu simu zao wakiwa kanisani

Lakini kasisi Don Michele Madonna, anakana kwamba kifaa chake kinatatiza shughuli za wenye maduka akisema kinaathiri tu mawasiliano kwa simu kwa waumini walio kanisani peke yake.

'Nilinunua kifaa hicho kutoka kwa duka la vifaa vya elektroniki, na kuwauliza polisi ikiwa ilikuwa sawa kuweka kifaa hiicho kanisani mwangu. Ni kifaa kizuri sana kwa sababu kimemaliza tatizo la watu kupigiwa simu na kuzipokea wakiwa kanisani.

Mmiliki mmoja wa maduka alisema: 'Tangu kasisi Madonna kuweka kifaa hicho ndani ya kanisa , nimepata matatizo sana kutumia kadi yangu katika biashara yangu. ''

'Kadi hii haifanyi kazi vyema na ninapoteza sana pesa zangu.''Kanisa la kasisi Don

Kasisi Michele Madonna aliamua kuchukua msimamo huo kwa sababu waumini walikuwa na mazoea ya kutumia simu zao kanisani wakati kasisi huyo akihubiri. Kilichomuudhi zaidi kasisi huyo ni watu kupokea simu kanisani na hata wakati wa mazishi.

Kasisi Don alinunua kifaa hicho kwa dola sitini.

Kabla ya kukinunua kifaa hicho alianza kwa kuwasihi waumini kutotumia simu zao kanisani kwa sababu zilitatiza shughuli zake. Alianza kwa kuweka mabango kanisani humo lakini ujumbe huo wengi hawakuuzingatia na hapo ndipo akalazimika kuweka kifaa hicho ambacho kinazuia watu kupokea au hata kutumia simu zao kanisani.

 
Top