Mwigizaji na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba ameibuka na kukanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo. Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost mwenyewe baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi. "Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe juzi nilikunywa --------- mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho.





 
Top