Kikosi cha Kabanga Eleven Fighters
Jana Jumapili ya tarehe 21/12/2014 katika uwanja wa Kabanga eleven Fighters uliopo Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera ulichezwa mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya Kabanga Eleven Fighters na timu ya Rubenga fc kutoka Giteranyi nchini Burundi. Katika mchezo huo Timu ya Kabanga Eleven fighters iliibuka na ushindi wa gori tatu kwa bila , magori yaliyofungwa na Mussa John mawili na Ezra Essau gori moja, magori yote yalifungwa kipindi cha pili cha mchezo huo.
Timu ya Rubenga fc
Aidha jana Jumapili ya tarehe 21/12/2014 katika uwanja wa Rulenge ulichezwa mchezo wa kirafiki kati ya Rulenge.com na Kabanga boys, katika mchezo huo timu zote mbili zilitoka sare ya kufungana magori matatu kwa matatu, mtandao wetu ulibahatika kupata majina ya mafungaji wa timu ya Kabanga boys ambapo magori yao yalifungwa na Issa Sako, Paul na Lazoro kila mmoja alifunga gori moja moja.
Wachezaji wa kabanga boys wakijipongeza baada ya mechi
Aidha hapo hapo Rulenge kulikuwa na mchezo mwingine ya kirafiki wa mpira wa wavu(Volleyball) katika ya timu ya spikers kutoka Kabanga na timu ya volleybaal ya Rulenge. Katika mchezo huo timu ya Spikers ya Kabanga iliibuka na ushindi wa set mbili kwa Moja. Aidha timu hiyo ya Spikers ilifuta makosa baada ya kupoteza mchezo wa kirafiki waliocheza Jumamosi ya tarehe 20/12/2014 dhidi ya timu ya volleyball ya Ngara ambapo katika mchezo huo timu ya volleyball ya Ngara iliibuka na ushindi wa set mbili kwa moja.
Rubenga fc kutoka Burundi


Wachezaji wa Kabanga boys wakijipongeza kwa vinywaji baada ya mchezo huo



 
Top