Msanii Mr Blue akiwa na rapa mkongwe na Mbunge wa Mbeya mjini Mr two Sugu.

Mbunge wa Mbeya mjini na msanii wa miondoko ya Hip Hop Joseph Mbilinyi amefunguka na kusema kuwa msaniiii Mr Blue amemfanya sasa arudi studio na kufanya nae kazi mpya iliyofanyika katika studio za Mj Records chini ya mtayarishaji
Markochali,Sugu amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kusema kuwa wimbo huo ni wimbo mkali sanaa na umepewa jina la Fredom.

"Mr Blue took me back to the studio leo (Jana),tumerekodi track yake mpya inaitwa 'Freedom'... Ni noma sana!"

Kwa upande wake Mr Blue amefunguka na kusema kuwa amefurahi sana kufanya kazi na mtu ambae anamuheshimu katika tasnia ya muziki kwa sababu Mr two ndio alimuhamasisha yeye kufanya muziki na kuweza kufanya poa zaidi katika sanaa kwa vitu alivyojifunza kwake.

"Nyandu tozzi na Joseph Mbilinyi kwa makochali kaa tayari shabiki wangu,nimefurahi sana kufanya kazi na mr two ni moja ya kaka zangu ninaowaheshimu na walionifanya niingie kwenye sanaa..leo (Jana) niko nae Alhamdulilahi kazi zinaendelea.."

Mwaka jana Mr Blue aliahidi kurudi rasmi katika muziki na kufanya juu chini kufanya kazi nzuri baada ya kugundua kuwa mashabiki wake bado wanamkubali na kumuelewa sana na hilo aliweza kujifunza na kushuhudia kila alipokwenda kufanya show maana alionekana kukubarika zaidi ya wasanii ambao walikuwa wakitamba na nyimbo zao kwa wakati ule.


 
Top