Kimekuwa ni kipindi cha majonzi kwa familia ya Mama Nyerere baada ya kuondokewa na kipenzi cha familia John Nyerere siku ya hivi karibuni. Kufuatia kujitoa kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa bila kujali itikadi za vyama vyao na watu mbalimbali kuifariji familia hiyo, Ndugu Charles Makongoro Nyerere alikuwa na maneno machache juu ya upendo ulioonyeshwa na jamii ya Kitanzania.

"Asanteni sana wote mliokuja kutufariji kama familia na wale mnaoendelea kujaasanteni sana. Mwili wa marehemu John Nyerere, umeishawasili nyumbani Msasani , heshima za mwisho zinaendelea kutolewa kwa mjibu wa ratiba. Hatuna cha kuwalipa wote kwa kutufariji hata kwa ujumbe, mungu awabariki sana."

 
Top