Kocha Mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal, akiteta jambo na staa wake Angel Di Maria 
Man United ililipa Euro 82 milioni kumtaka staa huyo kutoka Real Madrid, Agosti mwaka jana lakini ameshindwa kung’ara na kufikia matarajio ya kikosi hicho.

KOCHA Mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal amemweka wazi staa wake Angel Di Maria kwamba anapaswa kubadili tabia kama anataka kuwa mchezaji wa maana Old Trafford.

Man United ililipa Euro 82 milioni kumtaka staa huyo kutoka Real Madrid, Agosti mwaka jana lakini ameshindwa kung’ara na kufikia matarajio ya kikosi hicho.

Tangu alipotolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Arsenal Machi mwaka huu, Di Maria amekuwa akianzia benchi katika michezo minane mfululizo na kocha Van Gaal alifichua hilo limetokana na mchezaji huyo kutokuwa na hasira ya kutaka kubadili kiwango chake.

Van Gaal amemwambia mchezaji huyo anapaswa kubadili tabia yake na kuwa mpambanaji kama anataka kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

“Wachezaji ni lazima wazoee falsafa zangu na Di Maria ni lazima afanye hivyo,” alisema Mdachi huyo kwenye mkutano na waandishi wa habari juzi Jumamosi.

“Najua bado ana nafasi ya kulifanyia kazi hilo kwa sababu kila mchezaji anaweza katika mitazamo yangu. Kama unapojiweka wazi kwa kocha utaweza, lakini kama hutaki kukubali basi huwezi kubadilika.

“Si kwamba Di Maria hana kiwango, anacho na anaweza kucheza anavyotaka. Lakini mimi nina falsafa zangu na nataka wachezaji wazifuate. Hivyo ndivyo tunavyotaka kucheza kama timu.”


 
Top