MAJENGO YA MAABARA KATIKA KATA YA ILEMELA CHATO

Wananchi wa kata ya Ilemela Wilayani Chato Mkoani Geita wamegoma kuchangia ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Ilemela wakishinikiza serikali ichukue hatua dhidi ya watendaji waliofuja fedha za mradi wa ujenzi huo
Kauli hiyo wameitoa jana baada ya kuahirishwa kwa kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hiyo iliyokuwa imeitishwa kwa ajili ya kumaliza mgogoro huo kati ya wananchi hao na watendaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

Katika mgogoro huo mkuu wa Wilaya ya Chato Rudovick Mpogolo amesema kamati yake ya ulinzi na usalama imefika kwenye kata hiyo na kukuta mgogoro huo uliosababisha kukwama kwa ujenzi wa maabara hiyo ambayo imeagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amalize haraka tatizo hilo

Hata hivyo Mkurugenzi huyo Clement Belege amegoma kuzungumzia swala hilo kwa madai hawezi kulizungumzia huku akitaka wanahabari wachukue taarifa kwa mtoa habari wa awali aliyewapa kuwepo kwa mgogoro huo katika kata hiyo
DIWANI WA KATA YA CHATO ISMAIL LUGE.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya Ilemela Ismail Luge amesema wananchi hao wamegoma kuendelea na ujenzi huo baada ya Halmashauri ya Wilaya kuwakingia kifua watendaji waliofuja matumizi ya ujenzi huo ikiwemo kupotea kwa nondo na saruji

Hivi karibuni serikali kupitia agizo la waziri mkuu Mizengo Pinda imewaongeza muda wa kumaliza ujenzi huo wa maabara kutoka mwezi wa 12 mwaka jana hadi kufikia Juni 30 mwaka huu ndio mwisho wa ujenzi wa maabara kwa nchi nzima.

Chanzo: Kijukuu  Blog

 
Top