Pichani juu na chini ni Muonekano wa Nyumba yenye thamani isiyotambulika mara moja mali ya Bw Aron Rugamira imeteketea kwa moto katika Kitongoji cha Kumzenga kwenye mamlaka ya Mji wa Ngara Mkoani Kagera  June 27, 2015,majira ya saa saba mchana.
Miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo Bw Moses Rusasa alisema moto huo ulitokea kwenye chumba kilichokuwa hakijaunganishwa na nishati ya umeme na kwamba halijasababisha madhara ya kiafya kwa mtu yeyote na kwamba asilimia kubwa ya mali alizokuwa akimiliki zimeteketea kwa moto.
Kwa upande wake mmiliki wa nyumba hiyo Bw Aroa Rugamira akizungumza na Radio Kwizera iliyofika eneo la tukio, alisema tukio hilo wakati likitokea hakuwepo nyumbani kwake na alikuwa kwenye shughuli zake za Kijamii.







 
Top