Jengo la polisi likiteketea kwa moto
Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunju B wakiwa wamefunga barabara hiyo baada ya kugongwa kwa mwanafunzi Mwenzao aliyefahamika kwa jina la Omari na kufariki dunia leo hii.

Baadhi ya wakazi wa Bunju wamevamia na kukichoma moto kituo cha polisi Bunju A baada ya polisi kufyatua mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wananchi waliofunga barabara baada ya mwanafunzi na kugongwa gari na kufariki.

Polisi walilazimika kukimbia na gari lao baada ya kuona wananchi wanawazidi nguvu kwa kurusha mawe na kukiacha kituo hicho bila ya ulinzi ndipo wananchi walipokivamia kituo kuvunja milango na kuwatoa wahalifu waliokuwa wakishikiliwa na kisha kukichoma.

Inaelezwa kuwa kisa hasa cha watu kuamua hivyo inatokana na tukio la ajali ambapo mtoto mmojaRadhia Omary, mwanafunzi wa Shule ya Msingi kugongwa na gari

Askari wa Kituo hicho cha Polisi wamekimbia baada ya watu wengi kuvamia Kituo hicho na kuanza kukichoma moto… watu wanadai wameamua kufanya hivyo kwa kuwa sio mara ya kwanza tukio la ajali ya aina hiyo kutokea.” 

Chanzo:ITV

 
Top