Rais wa Tunisia ameapa kuimarisha usalama wa nchi

Washukiwa 12 wamekamatwa nchini Tunisia kwa kuhusika na shambulio katika hoteli ya kifahari eneo la Sousse.
Maafisa wa usalama wanaendelea kuwasaka washukiwa wengine wawili wanaodaiwa kupokea mafunzo ya kivita nchini Libya, pamoja na mshambuliaji wa hoteli hiyo.Kuna hofu huenda shambulio hilo likayumbisha sekta ya utalii

Wengi wa waliouawa katika hoteli hiyo walikuwa watalii kutoka Uingereza na wenzao kutoka Ulaya.

Wapiganaji wanaojiita Islamic State wamekiri kuhusika na shambulio hilo.

Serikali ya Tunisia inahofia shambulio hilo litayumbisha sekta ya utalii inayotegemewa kuletea nchi kipato cha nje.

Hapo mwezi Machi watu wawili waliokua na silaha waliwaua watu 22 katika makavazi mashuhuri ya Bardo mjini Tunis.

Mwanafunzi wa miaka 28 Seifeddine Rezgui ndiye aliyefanya shambulio hilo.

Credit:BBC

 
Top