Waziri mkuu wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa afanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya DSM leo tarehe 27/11/2015 na kukuta uozo hivyo kuagiza waliohusika na upotevu wa makontena 349 kukamatwa mara moja. Baadhi ya maafisa wa TRA wametakiwa kusalimisha hati zao za kusafiria maana wanahusika na uozo huo wa kontena 349 zilizokuwa na thamani ya bilion 80 ambayo data za mamlaka ya bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hazionekani.