Rais Dk. John Magufuli, amesema hakuna mfanyabiashara aliyemchangia kumuwezesha kuingia Ikulu katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Rais Dk. John Magufuli, amesema hakuna mfanyabiashara aliyemchangia kumuwezesha kuingia Ikulu katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu. "Nilijiepusha na fedha au mchango wowote kutoka kwa wafanyabiashara, kama yupo mfanyabiashara yeyote alinichangia hata shilingi mbili asimame hapa aseme, nilikwepa kwa sababu nilitaka iwe kazi tu," alisema jana wakati akiongea na viongozi wa sekta binafsi nchini.

Alisema wakati wa kampeni hadi kufikia siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu, hakupokea senti yoyote kutoka kwa wafanyabiashara kwa kuwa alijua akiingia madarakani anakwenda kufanya kazi tu.

Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wa sekta binafsi, katika kikao cha pamoja kilichoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) kwa ajili ya kufahamiana.

CHANZO:EATV
 
Top