Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

JAJI Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama alishinda atashinda tena kutokana na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa watampIgia kura tena.
Boman ameyasema hayo leo jijini Dar eS Salaam , wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Maalim kujitangazia kuwa ameshinda ni suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo kutokana na mazingira hayo uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya Zanzibar.

“Kurudia uchaguzi Zanzibar ni jambo lisilo epukika lakini wakae na kuangalia dosari zilizojitokeza na kufuta uchaguzi lazima lishughukiwe kisheria bila kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo”amesema Jaji Mstaafu, Boman.

Amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar walitakiwa kukaa na kuona wapi walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo ilikuwa ngumu kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha na wajumbe walishindwa kuafikiana.

Hata hivyo Boman ametaka suala la katiba lazima lishughulikiwe kuacha kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni ya fedha yametumika katika mchakato huo.

Amesema kuwa migogoro inayotokea ya ardhi na wafugaji pamoja wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo ndio ingekuwa suluhu ya utatuzi wa migogoro hiyo.
 
Top