Wafanyabiashara na wakazi wa eneo la Kabanga lililo jirani na choo cha jumuiya cha mji huo mdogo wilayani Ngara wanakerwa na hali ya uchafu wa choo hicho unapolekea kuwepo kwa harufu mbaya inayopelekea wafanyabiashara hao, kushindwa kufanya biashara zao katika hali nzuri ya hewa.

Akiongea na mtandao wa ngarayetu mmoja wa wafanyabiashara amesema kidogo leo tarehe 14/12/2015 hali kidogo ni nzuri baada ya malalamiko ya kipindi kirefu ambapo muhusika wa usafi wa choo hicho amesafisha na kuweka dawa hali iliyopelekea kupungua kwa harufu mbaya ilokuwa inachafua eneo linalozunguka choo hicho.

Wafanyabiashara na wakazi wameshauri juu ya choo hicho kwamba, mhusika achukue jukumu la kuhakikisha kinafanyiwa usafi kila siku na kila mara ili kuweka mazingira safi na kuwaondolea adha ya harufu mbaya inayowatesa na kuwasumbua katika majukumu yao na isiwe mpaka walalamike ndipo achukue hatua ukizingatia kwa hali ya sasa nchi inapambana na kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu unaoenezwa na inzi wanaopendelea uchafu.
 
Top