Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 07/12/2015 siku ya jumatatu ambapo mkuu wa wilaya Bi. Honoratha Chitanda na viongozi wengine wa wilaya wametembelea kata ya kabanga eneo la mji mdogo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuhimiza kampeni ya kufanya usafi inayoendelea wilayani humo na taifa zima kwa ujumla.

Mara alipowasili eneo la kabanga ameanza na zoezi la kuokota takataka zilizo zagaa akishirikiana na wananchi ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni ya usafi aliyoizindua siku ya Jumamosi ya tarehe 05/12/2015 katika eneo la Kojifa wilayani Ngara.

Mkutano wa mkuu wa wilaya huyo umeanza kwa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ambapo baadhi ya wakazi wa mji wa kabanga wameeleza kero zao mbalimbali zinazo wakabili. Mwinjiristi Jacob Kilula ameeleza tatizo la kutumia stendi ya magari ambayo ipo eneo lenye mgogoro wa ardhi, akifatiwa na mwijiristi Samwel George ambaye pia ni muwakilishi wa wafanyabiaashara wa kabanga amezungumzia kero ya vizuizi vya barabarani hasa kwenye barabara wanazotumia wateja wao kusafirishia mizigo pia ameongezea suala ya kufanya usajiri wa vyombo vya moto kulitoa mkoani na kulifanya liweze kufanyika katika idara za TRA zilizopo wilaya Ngara ili kuondoa adha ya watu kusafiri hadi mkoani kufanya usajiri. 

Bwana Nestori Bisabiko ameongelea kero ya kutopewa hati miliki ya viwanja na kudai kwamba gharama za kupima kiwanja ni kubwa hivyo zinamfanya mwananchi ashindwe kupimiwa kiwanja na hivyo kukosa mambo muhimu kama udhamini hasa pale anapoweza kutumia kiwanja chake kumdhamini, akiendelea kuongea ,ameongelea suala la mapato ya mnara wa Airtel ambapo mwanzo ulikuwa unaleta mapato kwenye kijiji lakini kwa sasa kijiji hakipati mapato hayo.  Hali kadharika mfanyabiashara bwana Fadhiri Nuhu ameomba suala la stendi lifanyiwe maboresho ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa vyoo. Pia wachoma mishikaki wameomba watolewe ufafanuzi juu ya zuio lililotolewa la kuwazuia kuendelea na biashara hiyo kwa sasa hadi aple watakaporuhusiwa tena. Na mengine mengi ikiwa ni pamoja na ushauri vimetolewa kwa mkuu wa wilaya huyo.

Yametolewa majibu juu ya kero hizo za wananchi, akijibu Afisa Tarafa amesema juu ya suala la vizuizi kwa wabeba mizigo hasa kwa baiskeli kuwa litafanyika zoezi la kusajiri waendesha baiskeli wote litakalofanyika chini ya ushirikiano wa viongozi wa vitongoji, vijiji, kata na jeshi la polisi, amesema kuwa mwendesha baiskeli atapewa barua ya utambulisho na kiongozi wa kitongoji itakayopitishwa na uongozi wa kijiji na kata na mwisho kitambulisho hicho kitamuwezesha kwenda polisi kuchukua namba itakayokuwa inamtambulisha hili litasaidia hata kuweka mizigo ya watu katika hali ya usalama. Pia ameomba kijiji ili kuondoa mgogoro wa eneo maarufu kama kimilamila lenye makazi ya watu linalotambulika kama eneo la shule kwenye ramani ameshauri libadilishwe na kuwa eneo la makazi ili kuepusha mgogoro wa hapo baadae hivyo kuiomba serikali ya kijiji kutafuta eneo jingine kwa ajili ya shule.

Zoezi la kutoa majibu likiendelea afisa usafi na mazingira wa wilaya aliyemuwakilisha mkurugenzi amesema, mgogoro wa stendi upo hivyo eneo lenye mgogoro halipaswi kuendelezwa kama kujenga miundombinu labda hayo yatafanyika baada ya maamuzi ya mgogoro huo kupatiwa majibu sahihi. Akiongelea suala la vizuizi amesema kuwa kwa sababu za kiusalama vizuizi hivyo haviwezi kuondolewa haraka bila kukaa na kufikiria kwa kina njia nyingine mbadala ya kufanya. Pia amesema watoto wa mtaani watakamtawa na kurudishwa kwao chini ya idara ya maendeleo na ustawi wa jamii kwa kushirikiana na wananchi. Pia kwenye suala la kukusanya mapato ya mnara amesema ni haki kwa halmashauri kufanya hivyo japo halmashauri inapswa kurejesha asimia kadhaa kwenye kijiji husika, hivyo amelipeleka kwa mkurugenzi ili kijiji cha kabanga kiweze kupatiwa 20% ya mapato ya mnara huo wa Airtel ulojengwa eneo la kijiji. Ombi la kupimwa viwanja , suala la barabara za mitaa na usajiri wa pikipiki ameyachukua hivyo atayafikisha kwa mkurugenzi ili yapatiwe majibu.

Kaimu afisa afya wa wilaya ndugu Robert Lutengelela amesema kampeni ya usafi wilaya Ngara ilizinduliwa tarehe 05/12/2015 katika eneo la Kojifa na mkuu wa wilaya na hivyo ili kuepuka na kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu wilayani Ngara pombe za kienyeji, uchomaji nyama (mishikaki) na uuzaji wa vyakula kiholela vimepigwa marufuku mpaka hapo watakaporuhusu tena.

Akihitimisha mkutano huo mkuu wa wilaya Bi. Honoratha Chitanda amesema sheria ya vileo iko palepale hivyo wauzaji wa vilevi wanapaswa kuzingatia muda uliopangwa wa kufanya biashara hiyo. Pia amesema vijana wanaoamkia vijiweni watakamatwa ili wapelekwe eneo linalowastahili kufanya kazi kwa lazima. Pia amesema kuwa stendi iliyopo haifai kwanza ina mgogoro pili ipo kwenye hifadhi ya barabara hivyo amesema stendi itatafutiwa eneo la kutosha litakalotengenezwa vizuri na kujengwa vyoo vizuri vya kisasa. Kuhusu vyombo vya moto kusajiriwa wilayani Ngara amesema hilo atalifanyia kazi kuhakikisha kuwa usajiri huo unafanyikia hapa hapa wilayani Ngara. 

Kuhusu vizuizi amesema vitaendelea kutumika maana nchi kwa sasa inategemea kodi ukizingatia kuanzia mwakani wanafunzi kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne sekondari watasoma bure hivyo kodi hiyo ndio italipia gharama hizo. Pia amesema utafanyika msako wa kukamata watoto wa mtaani na kuwarudisha kwao na pia ameshauri walau kila kaya kuwekeza kwenye kilimo cha maparachichi ili kujipatia kipato maana kwa sasa maparachichi yana soko sana nje ya wilaya ya Ngara. Mwisho amewashuruku wananchi na kuwataka wawe na ushirikiano mwema na serikali katika kuendeleza maendeleo ya nchi.

PICHA NA HABARI: EZRA ESSAU WhatsApp No. +255766378713







 
Top