Pichani ni mitambo mipya ya kufua umeme wilayani Ngara,mkoani Kagera,ikiendelea kufungwa na itakapokamilika itapunguza tatizo la mgao wa umeme kwa wakazi wa mji wa Ngara na maeneo jirani unatokana na uchakavu wa mitambo ya kufua umeme.
Mara baada ya kukamilisha ukarabati wa mashine hizo za kufua umeme zinazokadiliwa kuwa uwezo wa kuzalisha megawati 400.




Juu na chini ni Naibu Waziri Mwijage aliyevaa vizuia sauti kali masikioni,akikagua Mtambo wa kufua Umeme namba mbili wa shirika la umeme TANESCO wilayani Ngara mkoani Kagera.

Akifanya ziara wilayani Ngara,aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na MadiniMhe. Charles Mwijage alibainisha kuwa Wilaya ya Ngara ina mahitaji ya megawati 1200 za kutosheleza wananchi kupitia Tanesco lakini kutokana na uchakavu wa mitambo kunakuwepo mgao ambao unachangia wananchi kushindwa kuzalisha kiuchumi.

Hata hivyo amesema Serikali inafanya mchakato wa kuhakikisha wananchi wanatumia umeme wa gridi ya Taifa ikiwa ni pamoja na ule utakaozalishwa katika maporomoko ya Rusumo na kusambazwa katika nchi za Rwanda na Burundi.
 
Top