Mchezaji wa Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa Agosti 18 amefanikiwa kuifungia timu yake ya KRC Genk goli moja kwenye mchezo wa UEFA Europa League waliocheza dhidi ya Locomotiva Zagreb ya Croatia.
Kwenye mchezo huo wa kuwania kupangwa kwenye hatua ya makundi timu hizo zilifanikiwa kutoka sare ya kufungana goli 2-2.

KRC Genk ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao kwa njia ya Penalti kupitia kwa mchezaji wake raia wa Ubelgiji, Leon Bailey huku Samatta akiifungia timu yake hiyo bao la pili dakika ya 47. Zagreb ambao walikuwa nyumbani walifanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Mirko Marić kwa njia ya penalti dakika ya 52 na dakika ya 59 goli likifungwa na Ivan Fiolić.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana tena Agosti 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Cristal Arena unaomilikiwa na timu ya KRC Genk huku timu hiyo ikihitaji sare yoyote isiyozidi bao moja ili ipate nafasi ya kusonga mbele.
 
Top