Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera ,Luteni Kanali Michael Mtenjele amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuacha kunywa pombe saa za kazi na kutoa amri ya kukamatwa na kufikishwa Mahakamani haraka kwa tuhuma za uzembe na kukiuka amri halali ya Serikali kwa kunywa pombe saa za kazi ( kabla ya saa 9.30 alasiri ambao ndiyo muda wa kufunga ofisi za umma). Zoezi hilo kama litatekelezwa vyema,basi Wilaya ya Ngara mkoani Kagera itakuwa imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais John Magufuli kwa kuwasweka rumande watu wanaokutwa wakinywa pombe baa wakati wa saa za kazi.



Serikali ya Tanzania imepiga marufuku unywaji wa pombe, mchezo wa pool na michezo mingine wakati wa saa za kazi kama mkakati wa kuhakikisha kila Mtanzania anashiriki shughuli ya uzalishaji mali katika eneo lake.
 
Top