Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 31, 2017 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Sekondari, Kidato cha Nne kwa mwaka 2016, mtihani ambao ulifanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.44 ukilinganishwa na ule wa mwaka jana,2016.
Katika matokeo hayo, shule za Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam zimeonekana kung’ara zaidi kwa kushika nafasi za juu wakati huohuo shule 6 za Dar es Salaam zikishika nafasi 10 za mwisho katika matokeo hayo.

Shule zilizoingia 10 bora Kitaifa.

Feza Boys Sec School – Dar es Salaam
St. Francis Girls Sec School -Mbeya
Kaizirege Junior Sec School – Kagera
Marian Gilrs Sec School – Pwani
Marian Boys Sec School- Pwani
St. Aloysius Girls Sec School – Pwani
Shamsiye Boys Sec School – Dar es Salaam
Anuarite Girls Sec School- Kilimanjaro
Kifungilo Girls Sec School- Tanga
Thomas More Machrina Sec School – Dar es Salaam


Shule za Dar es Salaam zilizoshika nafasi 10 za mwisho.

Kitonga Sec School
Nyeburu Sec School
Mbopo Sec School
Mbondole Sec School
Somangila Day Sec School
Kidete Sec School

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60



 
Top