"Tuitake serikali itoe tamko la kuwarudisha watendaji hawa ambao ni darasa la saba makazini siyo kuwalipa, haiwezekani mtu amefanya kazi toka miaka mingi unakuja kumfukuza kazi, leo hatuzungumzi suala la kulipwa mafao bali warudishwe kazini watoke makazini kwa muda wao wa kustaafu na hili limefanyika hata kwenye majeshi, enzi hizo majeshini watu walikuwa wanachukuliwa darasa la saba leo wengine ni mameja, wengine ma OCD wameachwa mpaka wastaafu wenyewe iweje watendaji tunawafukuza kazi yaani mtu amebakisha miaka miwili ya kustaafu unamfukuza, tuiombe serikali na kama itakaidi mimi naomba na sisi wabunge wa darasa la saba humu ndani mtufukuze tu" Msukuma 



 
Top