Watoto wawili wa familia moja, Mussa Baraka (2) na Maiam Simoni (4) walifariki dunia kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba walimokuwa wamelala katika Mtaa wa Buguku eneo la Buhongwa jijini Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema watu watatu akiwamo mama mzazi wa watoto hao, Dabacha Simon; bibi yao, Linda Kulwa na kaka yao, Simon Samson (5) walijeruhiwa katika tukio hilo lililotokea saa nane usiku wa April 9,2018 na kulazwa katika hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ya Butimba.

Pia, Usiku wa kuamkia April 17,2018 mtu mmoja amefariki dunia baada ya nyumba yake kubomoka na kuanguka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Tukio hilo limetokea Kata ya Kiseke mtaa wa Kabambo Wilaya ya Ilemela. Aliyefariki ametambulika kwa jina moja la Laurent .
 
Top