Kabila
la hangaza au wahangaza ni kabila lililopo wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera
nchini Tanzania, ni kabila la watu wapole, wastaarabu na wakarimu kwa wageni. Ila
si vema leo tukajua asili ya neno au jina hangaza lilitokana na nini au wapi
lilitokea.
Kwa
historia ya mababu zetu ni kwamba hapo zamani kulikuwa na watemi wawili wa nchi
mbili tofauti yaani Burundi na Rwandakwa sasa , watemi hao walikuwa mtemi
Mwambutsa wa Burundi na mtemi Kigeri wa Rwanda. Watemi hao wawili walikuja
kupigana na mtemi Kinyamazinge wa Ngara. Watu wa Ngara walibuni vita ya
kupigania mpakani(boarder defensive) ambapo mababu zeetu walishinda mchana
kutwa wakikata miti na usiku ambao ndo ulikuwa muda wa vita walikoka moto mkubwa,
sasa wale warundi na wanyarwanda walipokuja kupigana vita vya ana kwa ana( full
force attack) walishangaa kuona Moto wakati muda huo wapiganaji wa ngara yaani
mababu zetu wakiwa tazama vizuri na kuwapiga mishale kwa urahisi sababu ya
mwanga wa moto ndipo neno hangaaza likiwa
na maana ya tazama kwa umakini kwa lugha ya Kiswahili lilianzia pale maana warundi
na wanyarwanda hawakuweza kuwaona vizuri wapiganaji wetu maana walikuwa kando
kidogo na moto huo hivyo wakawa wanaambiza hangaaza
neza ulibe yo bali yaani angalia kwa makini uone walipo kwa kiswahili . Na pia
kipindi hicho lilitumika zaidi kumaanisha mwanga wa vita kuanzia hapo wenzetu
wa Burundi na Rwanda baada ya kushindwa vita hiyo ndipo walipoanza kutuita
wahangaza. Na ndipo msemo wa kilugha
unasema utazi umhangaza amuhanga amaso ulipoanzia.