Mwanafunzi wa Chuo kikuu wa SAUT jijini Mwanza auawa na wanafunzi wenzake kwa tuhuma za wizi



Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini Mwanza, Helma Michael (22) akisomea ngazi ya cheti cha uandishi wa habari yaani CJM,na alifariki njiani akiwa anapelekwa hospitali.ameuawa kwa kupigwa mawe na wanafunzi wenzake, wakimhisi kuwa ni mwizi wa kompyuta ndogo za mkononi na deki chuoni hapo. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Valentino Mlowola, alisema juzi kuwa mwanafunzi huyo aliuawa Mei 13 mwaka huu saa 4.00 usiku, katika eneo la Nyamalango Malimbe, ambapo baada ya kubainika katika eneo hilo alianza kupigwa kwa mawe, fimbo na mapanga hadi kusababisha kifo chake: “Huyu
ameuawa katika tuhuma ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa,” alisema. 
Kutokana na mauaji hayo, watu 17 wamekamatwa na Polisi imeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo huku Kamanda Mlowola akiwataka watu kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu ambao hawana hatia.
Mwili wa marehemu Herman Michael aliefariki dunia tarehe 13/5/2014 umeagwa rasmi leo asubuhi kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro,
 
Top